Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, historia ya Marjaiyya ya Kishia katika kipindi cha miaka elfu moja kabla ya enzi ya Ayatollah Borujerdi imeshuhudia jumla ya mar'aji 58 wakubwa, ambao wengi wao walikuwa ni wairani waliopata elimu yao nchini Iraq. Katika kipindi cha Ayatollah Borujerdi, kutokana na juhudi zake pamoja na ubunifu katika nyanja ya elimu, uchapishaji na mawasiliano ya kimataifa, Hawza ya Qom iliingia katika mfumo mpya wa kimaendeleo na uboreshaji.
Katika kipindi cha miaka elfu moja hadi zama za Ayatollah Borujerdi, jumla ya mujitahidi 58 walitambuliwa rasmi kama mar'aj'i wakubwa wa kuigwa, ambapo 34 kati yao walikuwa ni wairani na 24 walikuwa ni Waarabu.
Kati ya mar'aj'i Waarabu, kumi na sita walikuwa kutoka Iraq, saba kutoka Syria, na mmoja kutoka Oman. Miongoni mwa mujitahidi 58 hao, arobaini walipata elimu yao Iraq, kumi na nne walipata elimu nchini Iran, na kuhusu wanne waliobaki haijulikani walipata elimu wapi.
Shughuli na Hatua za Ayatollah Borujerdi Kuhusu Hawza.
Rasul Jafarian, katika makala yake "Marjaiyya ya Kisiasa ya Kishia", ameripoti shughuli na hatua za Ayatollah Borujerdi kuhusu Hawza kama ifuatavyo:
1. Kuhusu usahihishaji na uchapishaji wa vitabu, ambavyo ni nyenzo za maendeleo ya Hawza. Kwa himizo kutoka kwa marehemu Borujerdi baadhi ya vitabu vya msingi vilivyo muhimu kwa wanafunzi vilichapishwa na kukabidhiwa kwao.
2. Kwa mujibu wa takwimu, idadi ya wanafunzi ilizidi kuongezeka, na ulipaji wa posho wa mara kwa mara uliandaa mazingira bora zaidi ya kujifunza kwa wanafunzi, kubaki Qom kwa ajili ya kuendeleza elimu, na kufikia ngazi za juu zaidi. Hata hivyo, kiasi cha posho hiyo kilikuwa kidogo kiasi kwamba hakiwezi kuhudumia kikamilifu maisha ya wanafunzi.
Jambo hili lilipelekea baadhi yao kuhamia miji mingine au kuajiriwa katika sekta ya elimu na vyuo vikuu.
3. Kuanzisha mawasiliano na Mashia wa nchi nyengine na kutuma wawakilishi katika baadhi ya nchi za Ulaya, wakiwemo "Bwana Muhammad Muhaqqiqi kwenda Ujerumani" na "Bwana Mahdi Haeri kwenda Marekani", ilikuwa ni ishara ya maendeleo ambayo Hawza ilikuwa imefikia.
4. Kuanzishwa kwa majarida kama; “Hikma”, “Maktaba Islam” na “Maktaba Tashayyu”, ambayo yote matatu yalikuwa na nafasi muhimu katika kuendeleza shughuli za uchapishaji, kulitokea katika kipindi hiki.
5. "Kuanzisha mawasiliano na wanazuoni wa Misri" na kushiriki katika kuanzishwa kwa "Dar al-Taqrib", pamoja na uwepo wa mwanazuoni aitwaye "Muhammad Taqi Qummi" katika kituo hicho, kulikuwa ni dalili ya kuenea kimataifa kwa fikra ya kidini na kimadhehebu ya maulamaa wa Kiislamu. Kabla ya wakati huu, hawakuwa na uwezo wa kushiriki katika shughuli kama hizo.
Jambo hili lilikuwa na athari kubwa katika kukuza fikra ya "umoja baina ya Sunni na Shia" katika maeneo ya maulamaa wa Kishia. Msingi wa fikra hii uliwekwa na Ayatollah Borujerdi, jambo ambalo halikuwa na mfano wake katika enzi za hivi karibuni katika ngazi ya Marjaiyya.
6. "Lililo muhimu zaidi ya yote ni kuimarisha nafasi ya dini na madhehebu katika jamii", jambo ambalo lilikuwa limeathirika vibaya katika enzi ya Reza Shah, sasa lilikuwa linarejeshwa. Marjaiyya ambayo katika miongo mitatu au minne iliyopita ilikuwa imepungua nguvu kwa sababu ya propaganda za watu waliokuwa wakiita kwa mwangaza wa fikra (monafeqīn) na kwa msaada wa utawala wa kidikteta, sasa ilikuwa inarejeshwa tena katika nafasi yake.
7. "Kulea kizazi cha wanazuoni mashuhuri", ambao wengi wao katika kipindi kilichofuata walichukua nafasi muhimu si tu kielimu bali pia kisiasa ndani ya Hawza. Moja ya hatua zilizochukuliwa katika kipindi hiki ilikuwa ni mafundisho ya tafsiri ya Qur'ani na falsafa ya "Allama Tabataba’i", "marehemu Sayyid Muhammad Muhaqqiq Damad" na pia "Imam Khomeini", yote haya yalikuwa na athari kubwa.
"Ustadh Shahid Murtaza Mutahhari" na "Imam Musa Sadr" ni mfano tu wa wanafunzi waliobobea katika Hawza hiyo, ambao wanafanana na wengine wengi waliopata malezi kama hayo. Marehemu Ayatollah Borujerdi pia alijishughulisha na kuimarisha Hawza katika miji mingine, na hatimae alianzisha shule moja huko Najaf.
Maoni yako